HIRIZI YA MAPENZI SEHEMU YA 2 - Chumba Cha Mapenzi -->

HIRIZI YA MAPENZI SEHEMU YA 2


Nilibaki nimepigwa na butwaa huku nikiachia mdomo wazi, sijui ni nani amenitumia ile sms na amejuaje kuwa mimi niko na Jacq hapa chumbani kwangu.
Akili ya haraka iliyonijia hapa ni kumtimua Jacq arudi kwao ili aniepushe na matatizo yanayokaribia kunikuta.
Ujumbe wa ile sms ulikuwa mzito sana, nisingeweza kuupotezea hata kidogo. Ila swali nililojiuliza “Ni vipi Jacq atalipokea hilo?”. Nilikuwa na hakika kuwa hatanielewa. Na pale simu yangu ilipoanguka na kuzima, mpigaji alifikiria nimemkatia simu, hivyo akazidi kupandwa na hasira.
Nikaamua nimuonyeshe Jacq ile sms ili nijue atasema nini.
“Anko Jose huyu, achana nae..” Ndivyo alivyoniambia Jacq huku akinikabidhi simu baada ya kusoma sms ile. 
“Hapana mpenzi, nawezaje kuachana nae wakati ujumbe ni mzito sana huu na wewe unajua maisha yangu tena yalivyo, na hapo pametajwa jela tayari” Nililalama ili angalau Jacq anisikilize na kunielewa, lakini ilikuwa kazi bure. 
“Hawawezi kukufanya chochote, wala usiwe na wasiwasi my” Jacq alisema kwa kujiamini.
“Kama ni hivyo basi washa simu yako ili wakutafute wewe na sio mimi” Nilimkazia Jacq kwakuwa hali ilishakuwa tata upande wangu. Tangu siku ya kwanza kuja hapa kwangu Jacq alizima simu yake, hakutaka apatikane.
“Simu mimi siwezi kuwasha maana bado nataka niendelee kukaa na wewe hapa, halafu hiyo mada ibadilishe” Ndivyo alivyonijibu Jacq na kugeukia pembeni. 
Nikakaa pale juu ya ile meza nikitafakari namna ya kulikabili janga lililopo mbele yangu muda huu. Sikuwa na namna ya kufanya.
★★★★★★★★★★★★★
Niliuangalia mwili wa Jacq uliokuwa umeumbika akiwa na kanga moja tu pale kitandani huku akiwa amenipa mgongo nimuone kwa nyuma. Nyuma palikuwa pamejazia vizuri kuliko maelezo, hisia za mapenzi zikapanda. Nikasahau kabisa kuwa nimepigiwa simu na watu wa kwao.
Nikaiweka simu pembeni kwenye ile meza, nikautupa mbali msuli niliokuwa nimejifunga kiunoni na kujirusha pale kitandani.
Nikaikagua vizuri ile kanga pasi na kuishika, nikafanikiwa kujua ilipoanzia. Haikuwa imefungwa, iliegeshwa tu, labda hii ilikuwa ni makusudi ili kumvutia mtazamaji. Nikaishusha taratibu na kuanza kumpapasa 'chura' wake. Akageuza uso kunitazama kisha akatabasamu. Mimi sikuongea chochote, nikajiweka 'busy' na kazi ile ambayo nimeianzisha.
Nikamgeuza na kukitazama kifua chake jinsi kilivyokaa vizuri. Hapa palikuwa na nido za wastani zilizosimama barabara. Rangi yake ya maji ya kunde ilinogesha zaidi muonekano wa hapa. Nikazamisha kichwa changu na kuanza 'kuzipiga ulimi'.
Hapa ndipo niliposikia mlango wa chumbani kwangu ukigongwa kwa nguvu sana. Nilishtuka na kuruka pale nilipokuwa. Nikarudishia msuli kiunoni kama mwanzoni na kuuendea mlango bila kutoa sauti yoyote. Mgongaji bado alikuwa anaendelea kugonga kwa nguvu. Safari hii akipiga makelele “Funguuaaaaa”. Nikakamata kitasa na kuzungusha funguo, kisha nikausukuma mlango kuelekea ndani ili kumfahamu mgongaji. 
Lahaulaaa... Sikuamini macho yangu. 
Alikuwa ni rafiki yangu kipenzi, Nira aliyekuwa pale mlangoni huku akitweta. Akataka kunisukuma niingie ndani nikakataa. 
“Tuyamalize tu hapa hapa kaka, ndani yupo shemeji yako humu” Nilimsihi.
“Hicho ndo kilichonileta, kaka uko hatarini” Aliniambia na kunifanya nishtuke kuliko kawaida. Ni kweli nilihisi kitu si cha kawaida kwa ujio wake ule, lakini kuhatarisha maisha yangu tena?! Hii sikuitegemea.
“Eeenh.. Ni nini hicho kaka?!, tatizo nini kaka? Nambie..” Nilisema kwa sauti ya juu sana, nilihisi kuchanganyikiwa.
Nira akanishika kichwa na kunivutia kwake na kulileta sikio langu usawa wa mdomo wake kisha akaninong'oneza.
“ Kaka, kimbia haraka, wazazi wake wanakuja na polisi”. 
“Jay mbona kelele, kuna nini mpenzi?” Ilikuwa ni sauti ya Jacq aliyekuja kwa nyuma na kunishika bega.
Nikamtazama kisha nikamtazama Nira bila kujua nijibu nini.
★★★★★★★★★★★★★

Itaendelea...