Jibu la Tanasha Kuhusu Kubadili Dini Kisa Diamond Platnumz
May 19, 2019
Edit
Mpenzi wa msanii Diamond Platnumz, Tanasha amesema kuwa si rahisi kwa yeye kubadilisha dini kisa mahusiano ila mapenzi yake na muimbaji uyo pale pale.
Tanasha amefunguka hayo alipokuwa akihojiwa na Wasafi FM kwa kueleza kuwa kila mmoja anaheshimu dini ya pande zote mbili.
"Mara ya kwanza nilikuwa na wasiwasi wakati tunaanza uhusiano, Diamond Platnumz ni star na nini. Naheshimu dini yake na yangu pia, sitabadilisha dini lakini mapenzi yatabaki," amesema Tanasha.