Hizi ndizo idadi ambazo Mwanaume hufikiria Mapenzi Kwa siku - Chumba Cha Mapenzi -->

Hizi ndizo idadi ambazo Mwanaume hufikiria Mapenzi Kwa siku

Umewahi kusikia kauli hizi? ” Mume wangu hatosheki kitandani..” “..Sidhani kufanya mapenzi ndio liwe jambo la msingi lakini huyu mwanaume kaa! Basi tu kila siku mpaka kero..”Bila shaka ni kilio cha wanawake wachache walioamua kusema. Hivi kweli ni mara ngapi au kiasi gani tuseme inatosha? Je wanaume wanafanya makusudi? Je kuna uwezekano wakabadilika?
Katika mapenzi, suala la kumtaka mwenza kimapenzi hutegemea sababu nyingi, chache ni uwezo wa kiafya, utayari wa kihisia, usalama wa kazini na mengineyo. Japokuwa jinsia zote huwa na kiu ya mapenzi lakini wanaume huwa ni zaidi.
Daktari David Reuben anasema kuwa “.. Wanaume wengi huzungukia ktk mzunguko wa saa 48 yaani huhitaji kukutana kimwili kila baada ya saa 48 ili wawe ktk hali njema ya kimwili na kiakili…”Nae Daktari na mwandishi Dr Herbert Miles anasema “.. Mwanaume mwenye afya njema mbegu hujaa kila baada ya saa 42 hadi 78 na kuzalisha nguvu kali inayohitaji zitolewe..”
Pia mwanasayansi Alan Frome anasema kuwa ‘.. Wanaume wanaonekana kuwa na njaa ya kukutana kimwili kwa sababu ya maumbile ambapo prostate gland ina kifuko kidogo kitunzacho mbegu, na kijaapo, mwanaume huhitaji kuzitoa, presha huzidi zaidi na zikitoka hurudi ktk hali yake ya kawaida..”