KWANINI TUPO DUNIANI???.....sababu za msingi kwann tupo duniani - Chumba Cha Mapenzi -->

KWANINI TUPO DUNIANI???.....sababu za msingi kwann tupo duniani


             KWANINI TUPO DUNIANI?
           Wanafalsafa wamekuwa na maswali mengi juu ya kuwepo kwa maisha duniani na ulimwengu kwa ujumla,wao huhoji ,nini chanzo cha mwanadamu? Nini chanzo cha ulimwengu? Je kuna Mungu kweli? Na kwanini tunaishi? Na maswali mengine mengi.
Nimekuwa nikifuatilia hoja mbalimbali za wanafarisafa nguli kama Aristotle,socrate,Plato, Charles Darwin,Isack Newton,John ray n.k pia wanasayansi na wanahistoria wanametafizikisi.
Wanaojaribu kuangalia ulimwengu ulianza ln kwann uko hv n.k nikabaini kuwa :
*wote wamekazana kuangalia asili au mwanzo wa ulimwengu na watu(origin).
*hoja zao zimezama kwenye nadhalia(kufikirika) tu si uhalisia, kama :kusema kuwa mwanadamu au viumbe wanatokana na maozo(spontaneous creation by Aristotle 384-322),  na Van Helmont(1557-1644) " au kusema mwanadam anatokana na muunganiko wa chemikali na shughuli za kifizikia(Biochemical evolution) au kusema mwanadamu alianzia juani mbegu ikaja duniani hadi baharini (Cosmozoan theory)n.k
*nyingi hazijabeba hoja za jumla kuhusu asili ya ulimwengu.utakuta hoja imezama katika kuelezea jambo moja tu maalumu kama: mwanzo wa mabara tu "continental drift ", na si ulimwengu wote au au mwanzo wa binadamu kama "man 's evolution" ambayo inaelezea asili ya mwanadamu tu na si viumbe wote, Dust cloud hypothesis na The big bag theory ambazo zinajaribu kuelezea asili ya dunia na si viumbe vyote n.k
*special creation pekee ndio inayoeleza kwa ustadi na systematic mwanzo wa ulimwengu -dunia,jua,wanyama,ndege,wadudu,wanadamu,sayari zote n.k.
Na ndio theori pekee ya kale na ya mwanzo,wakinaplato wameikuta,isck newton wameikuta n.k
Theori hii iliyoandikwa na Musa ,katika kitabu cha mwanzo sura ya kwanza, imeenda mbali na kutueleza kwnn tupo duniani.
Wanasayansi hawajiulizi kwnn mwanadamu yupo duniani kwani siku wakijiuliza hilo wataokoka
Pia wameshindwa kujiuliza kwnn tunakufa na ilikuwaje tukaanza kufa?
 Mimi nitapenda kujibu maswali haya kwa kutumia maandiko matakatifu hasa Biblia kujibu swali hili la kwanini tupo duniani?Nikianza mwanzo kabisa mwa uumbaji wa mwanadamu wa kwanza hasa kwa kulitazama kusudi la Muuumbaji mwenyewe kumuumba mtu,kwanza ,ninagundua kuwa mwanadamu aliumbwa ili avitawale viumbe vingine ,lakini pia nikisonga mbele ninakuta lengo la pili kuwa ,alimuumba ili akaijaze nchi(rejea Mwanzo 1:26-28).
Lakini jambo lingine la tatu ni kwa ajiri ya kumwabudu Mungu.Mungu hakumwacha tu mwanadamu afanye kama atakavyo yeye au aishi atakavyo yeye alimwekea  sheria ili aishi katika hizo(mwanzo 2:15-17)
 Lakini nimekuwa nikijiuliza zaidi hasa ninapoendelea kujifunza maandiko zaidi kuwa,kwanini kuwe na mwisho wa dunia? Inakuwaje Mungu aumbe ulimwengu harafu baadaye auteketeze huo ulimwengu na kutokeza ulimwengu mwingine? Kwanini kuna ukomo wa maisha ya mwandamu?
            Baada ya kutafuta sana kwa kuyachunguza maandiko nilianza kubaini kuwa ,mwanzo kabisa Mungu alipenda aishi pamoja na mwanadamu ,ndiyo maana alimweka katika bustani yake na alikuwa akimtembelea(mwanz 3:8).Lakini Mungu alitaka mwanadamu aishi milele,ndiyo maana anamkataza Adamu asile tunda lile la ujuzi wa mema na mabaya kwani akila atakufa ,na kinyume chake kuwa asingekula asingekufa hakika(Mwanz 2:7).
 Lakini nikaenda mbali kwa kuyatafuta majibu ya kwanini kuwe na mwisho wa dunia? Au kwanini Mungu anaenda kuifumua mbingu na nchi na kufanyiza mpya?,ukisoma  katika ,2pet 3:10-11,imeandikwaLakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi;katika siku hiyo mbingu zitatoweka  kwa mshindo mkuu,na viumbe vya asili vitaunguzwa,na kufumuliwa,na nchi na kazi zilizomo ndani yake kuteketea.Basi,kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo,,,.Pia katika Ufunuo 21:1 ,imeandikwa Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya ;kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita ,wala hapana habari tena.
            Nilibaini kuwa matokeo ya dhambi yaliweze kubadilisha kusudi zima la Mungu la kumuumba mwanadamu aishi duniani,kwanza, mwanadamu alianza kuwa na ukomo wa kuwa katika dunia hii,na pili kukaibuka mwisho wa duniani hii ili kumwadhibu shetani na mwanadamu aliyekataa kuishi kama Mungu alivyomwagiza.
Maana yake nini? Mwanadamu asingetenda dhambi kusingekuwa na hukumu ya mwanadamu ,ni shetani pekee angehukumiwa pamoja na kikundi chake au malaika zake(Mathayo 25:41).
 Lakini nikazidi katika kutafakari sana ,kuwa, kwanini Mungu hakuikomesha dhambi kwa kumwangamiza shetani? Au kwa kuwafanya wanadamu wamtii kwani yeye aweza yote?
            Pia,kwanini mwandamu anaendelea kuzaliwa na idadi yake inazidi kuwa kubwa wakati kuna mwisho wa dunia?
 Mpendwa unayesoma makala hii,ninakusihi kwa jian la Yesu kuwa usome  kwa jian la Yesu Kristo ukaelewe nini Mungu anataka  kuongea na wewe.
 Katika kusoma maandiko matakatifu nilikuta sehemu fulani zimeandikwa kuwa yeye ashindaye nitampa kula matunda  yamti wa uzima ,ulio katika bustani ya Mungu Ufunuo 2:7b,pia  Yeye ashindaye,nitampa kuketi pamoja  pamoja nami katika kiti changucha enzi,kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na baba yangu katika kiti cha enziUfunuo 3:21 na  Basi  na sisi pia ,kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii,na tuweke kando kila mzigo mzito,na dhambi il ituzingayo kwa upesi:na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu.ebrania 12:1,unaweza kusoma  zaidi katika ,Ufunuo 2:11,1726,3:5,12 na Uf 21:7.
 Hapa ndipo nikabaini kuwa ,kumbe tupo duniani kushindania uzima wa milele.Pamoja na jitihada zetu zote ,mafanikio yetu yote ,kutaabika na kuhangaika kote lakini lengo kubwa la kuwa duniani ni kwa ajri ya kushindania uzima wa milele.
Ndiyo maana Yesu anasema kuwa wale watakaomwamini watapata uzima wa milele(Yohana 3:16) na sehemu nyingine anasema anaenda kutuandalia makazi na atakuja kutuchukua tena (Yohana 14:)).Lakini mtume Paulo anabainisha kuwa makazi yetu sisi yako Mbinguni(Wafilipi 3:20) na mtume Petro yeye anasema kuwa ,tu wapitaji na wasafiri katika dunia hii(1 Pet 2:11)
             Watu wengi wamepotoka  kwa kuamini kuwa  duniani ni mahari pa starehe,kufanya uzinzi,kuwa na wanawake wengi,kulewa na kujifurahisha nafsi kote.Wapendwa katika Kristo siku hizi katika ulimwengu uliojaa  elimu,ujuzi wa  hali ya juu na uhitaji ,wanadamu kila siku huamuka wakiwaza wafanyeji ili wapate mahitaji yao hasa pesa kwa ajiri ya kujikimu kimaisha.
Nenda kwenye vyuo mbalimbali utakutana na watu wengi ,vijana kwa wazee,wa kiume na wa kike, kila mmoja akipigana ili afaulu.lengo ni kupata ajira ili kutimiza ndoto zake kama, kuwa na nyumba nzuri ,kuwa na gari na kuwasaidia wanyonge.
Pia unaweza kutembelea katika stesheni mbalimbali za mabasi na gari moshi pia na uwanya wa ndege,huko nako utakutana na watu wengi wakisafiri kwa ajiri ya kwenda kuwaona ndugu, jamaa na rafiki,kibiashara na wengine kihuduma.
Tembelea pia kwenye masoko ya nguo na vyakula,baa ,hotelini na kwenye migahawa ,huko nako utakutana na watu wengi ,kila mtu akijibidisha ili atimize haja yake.
Lakini ipo hatari sana katika haya kwani watu wamesahaulishwa na mahitaji ya mwili na dunia kwa ujumla ,wakisahau kusudi la wao kuja hapa,kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyotahadharisha kuwaBasi,jiangalieni,mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi,na ulevi,na masumbufu ya maisha haya;siku ile ikawajilia ghafula ,kama mtego unasavyo Luka 21:34.
Tumekuja duniani kutafuta tiketi ya kuishi peponi au kuishi maisha ya mateso jehanamu.Hivyo duniani si sehemu ya kujivunia sana wala kungangania,bali ni sehemu ambayo mwanadamu anatakiwa kuwa makini sana kuusaka ulimwengu wa kiungu.Ndiyo maana Yesu anawataka watu wote wausake kwanza ufalme huo,kabla ya mambo mengine,kwani anasema kuwa mengine  ni yaziada tu(utajiri,elimu,cheo,ndoa n.k),haya yote tutayaacha hapahapa duniani,tutaondoka pasipo kujua,mali zote ,heshima zote vitabakia hapa hapa duniani na kupita.
 Inawezekana usielewe nini ninachokisema  kutokana na yale ambayo umekuwa ukiyaamini ,lakini hebu fuatilia viashiria hivi vinvyodokeza kusudi la mwanadamu kuwapo duniani,kama ifuatavyo,
            Jambo la kwanza,Hatima ya jitihada zetu,mfalme Suleiman alikuwa ni moja ya wafalme wa Israeli ambao ni maarufu sana,ni ngumu kueleza juu ya wafalme pasipo kumwongelea huyu,yeye anasifika sana kwa kujariwa hekima ambayo aliiomba kwa Mungu naye akampa,hata hivyo akapewa na utajiri mwingi.
Mfalme huyu kutokana na kuwa na hekima kubwa alitokea kuwa maarufu sana kati ya wafalme na kuwa tajiri sana,lakini pia alianza kufanya utafiti kuona kuwa ataweza kuitosheleza nafsi yake,anadai kuwa, alijitwalia wanawake wa kila aina,alipanda miti na maua ya kila namna na mambo mengine mengi(rejea Mhubiri2:1-11)).
Hata hivyo mwisho wa siku anakuja kubaini kuwa nafsi haishibi ,na kuona kuwa yote aliyoyafanya yalikuwa upuuzi mtupu kwani jhitihada zake zilikuwa bure ,mwisho wake atarudi mavumbini pasipo na kitu chochote alichokihangaikia kwa muda mrefu(Mh 5:13-15).
 Rafiki yangu aliniuliza swali ambalo  mwanzo nililiona kama anataka kunikejeli,baada ya kumweleza nia yangu ya kutaka kuanzisha taasisi,aliniuliza kuwa, kwanini ninataka kuanzisha taasi? Nikamjibu, ili kutimiza ndoto zangu.Akaniuliza tena ,ili iweje? Nikamwambia ,nipate faraja moyoni mwagu.Akazidisha swali ,harafu? Nikakosa jibu.Lengo lake lilikuwa si baya kama nilivyozania hapo mwanzo, baada ya kuja kutafakari sana,nikagundua kuwa alitaka kunidokeza kuwa ,yote nikayoyafanya niyafanye kwa ajiri ya utukufu wa Bwana ,kwani hiyo ndiyo itakayokuwa pona yangu.
            Hapa ndipo tunaweza kubaini kuwa ,kumbe yale ambayo tumekuwa tukiyahangaikia nakuhuzunika sana tunapoyakosa na pengine kumwacha hata Yesu ni kwasababu ya  kutusaidia twendelee kuwa hai mfano chakula,malazi na mavazi.Mtume paulo yeye anaona mambo ya mhimu ni chakula na mavazi,na kuongeza kwa kusema kuwa “…lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi,na tamaa nyingi zisizo na maana,zenye kudhuru,ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu 1th 6:6-10.
 Pili,udahaifu wa mwanadamu,ninapoonglea udahaifu, hapa ninamaanisha kuwepo kwa walemavu hasa vipofu,viwete,bubu  na viziwi na wanyonge wengine katika jamii yetu.
Hapo mwanzo nilikuwa nawasumbua sana wachungaji na watumishi wengine wa Mungu kwa kuwahoji kuwa ,je,Mungu hubagua? Kwanini kuwe na walemavu na wengine wasio walemavu?  Na hasa kwa kulitazama neno ambalo yeye mwenyewe Mungu alilisema ,akimwambia Musa katika Kutoka 4:11 ,kuwa                                  BWANA akamwambia,ni nani aliyekifanya kinywa  cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi,au mwenye kuona,au mwenye kipofu? Si mimi ,BWANA?.
 Hili swala lilinitesa sana,lakini Mungu mwenyewe kwa njia ya Roho wake alinifunulia siri hii kuwa ,Mungu hana ubaguzi wala upendeleo ,bali amemuumba kilema na asiye na kilema kwa ajili ya kumwabudu na kushindania uzima wa milele.Ndiyo maana tunaona kuwa tutakapoingia peponi hakutakuwa na mtu mwenye ulemavu, watu wote tutakuwa sawa,ukisoma Isaya 35:3-10, “…….ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa,na masikio ya viziwi yatazibuliwa.Ndipo mtu aliyekilema ataruka ruka kama Kulunga,na ulimi wake aliye bubu utaimba..
            Kwahiyo kila mtu analojukumu la kuusaka ufalme wa Mungu pasipo  kujali ni mlemavu au si mlemavu,kwani mlemavu kwa ulemavu wake anapaswa kuusaka ufalme wa Mungu na yule asiye mlemavu  kw a namna alivyo ,mzuri wa sura kwa uzuri wake na asiye mzuri kwa namna alivyo.
Hakuna asifaa kwa Mungu,wote anawapenda,ingawa wengine wamemdaharau Mungu na kujibadilisha sura na maumbile yao wakizani kuwa wameumbwa kwa ajili ya uzuri au zinaa,kumbe tumeumbwa kwa ajili kuusaka ufalme wa Mungu.Na, kwasababu ya upotovu wa mawazo yetu tunafikiria kuwa tumeumbwa kwa ajili ya ya kuipendezesha dunia badala ya kumpendeza Mungu.
Ndiyo maana wakati mwingine tunawacheka wadahaifu   tukizania tuliumbwa kwa ajili ya kuwa matajiri,wenye akili,wenye miguu na mikono,kumbe kwa ajili ya kuusaka ushindi.Utajiri ulionao kama ni wakutoka kwa bwana ,Mungu amekupa kwa ajili ya kutafutia ushindi,umasikini vilevile na ulemavu vile vile.
Pia,Kutoweka duniani,mwanadamu amekuwa akitoweka duniani pasipokujua,yaani kwa wakati asiouzania.Mwanadamu amekuwa hana uhuru wa kujua kuendelea kwake kuwepo duniani.Haijalishi anaumri kiasi gani,mtoto,kijana ama mzee,wote wanatoweka pasipo kujua.
Siku moja nikiwa jijini Arusha ,baba yangu mzazi alinipigia simu na kunipataarifa fulani,haikuwa taarifa njema hata kidogo, ilikuwa ni taarifa ya baba zangu wadogo kufariki wote wawili ndani ya mwezi mmoja,nilikuwa nawapenda sana,kwa kuwa nimewahi kuishia nao na katika maisha yangu ya shule walikuwa wananisaidia sana kwa kunifundisha wakati nikisoma shule ya msingi.
Mara kwa mara huwa nikisikia habari za vifo lakini,huwa ninachukulia kawaida, lakini siku hiyo,ilipenya hadi kwenye vyumba vya ndani vya moyo wangu,nililia utazania mtoto.Si kwamba nililia kwasababu yawale baba kufa , nililia kwakugundua kuwa kumbe maisha yetu ya duniani  nikama maua tu yanachanua na kunyauka.
Lakini pia mwaka 2012,nilikuwa katika wakati mgumu sana ,nyimbo za msanii mmoja hivi sasa ni marehemu anaitwa Fanueli sedekia zilikuwa faraja yangu kubwa sana,kwa bahati mbaya  sana nilipotaka kumfahamu zaidi nilipata taarifa kuwa tayari alikuwa amekufa,nilihuzunika sana,na kumhoji Mungu kwanini kumchukua mtu wa mhimu kama huyu?
Nikaja kubaini kuwa kila mtu ameumbwa kwa ajiri ya kusudi fulani ,kwa kipindi fulani  ,mahali fulani na kwa kiwago fulani na katika hayo kila  mtu ataweza kuhukumiwa kama aliweza kumcha Bwana akiwa katika kutimiza makusudi hayo.Kwa mfano kama ni mwimbaji ,uliwezezaji kumwimbia Mungu huku ukizishika sheria zake? Kwa hiyo muda wa hilo kusudi linapoisha ndipo mwisho wa mtu unapokuwa hutimia.Nakumbuka mwalimu Mwakasege akiwa katika viwanja vya furahisha jijini Mwanza akisimulia kifo cha Sedekia alisema kuwa, alijitahidi kumwombea sana kwa maombi ya kila namna ,hata hivyo upako wote ulikuwa unapukutika tu.
Akaenda mbali kwa kumwomba Mungu kuwa, kama hataki kumsikiliza yeye basi asikilize hata maombi ya watu wengine,kwani aliamini kuwa kuna watu walikuwa wakimwombea Sedekia.Pamoja na jitihada hizo ,Sedekia alipoteza uhai wake.
      Ndiyo maana  utashangaa kuona mtu alikuwa hai lakini anakufa ghafula,huyo safari ake imeshafika ukomo.Wapo wengine walijaribu kutaka  kutoshuka kwenye vituo vyao,madaktari walijitahidi kuokoa uhai wao kwa kuwawekea mitambo ya kupumulia,chakula na maji,na wengine kuweka moyo  wa bandia,vyote hivi vilishindikana,safari ikifika mwisho huwezi kulazimisha.Safari ikifika haichagui wewe ni nani? Una mali gani? Na una umri gani?
Nini nataka kudokeza hapa?
            Pamoja na kwamba tunaweza kuwapenda watu fulani na kutamani wabaki muda mrefu ili tuendelee kupata zile huduma ambazo tumekuwa tukizipata toka kwao,lakini tufahamu kuwa, kila mwanadamu ameumbiwa muda wa kukaa duniani akijaribu kutimiza kusudi fulani la Mungu kwa watu fulani.
Mtumishi moja alituuliza kuwa,kwanini unafikiri usingezaliwa miaka mia moja iliyopita? Au kwanini usingezaliwa nchi nyingine zaidi ya Tanzania?  Jibu ni kwamba ulikuwa si wakati wangu kwasababu ya kusudi langu kwa Mungu,kwa kiwango fulani na watu fulani.
Kwahiyo nikagundua kuwa ,kila mwandamu anapaswa kutafuta kujua kusudi la Mungu kwake yeye kuwepo hapa duniani.Mwanafalsafa mmoja yeye alisema kuwa every body in the world is for something and somebody kwa kiswahili kila mtu ulimwenguni yupo kwa ajiri ya kitu fulani na mtu fulani.Mwingine alisema kuwa the world is like a universty where different  people take different courses and every one is tested according to his/her  course ,kwa kiswahili ulimwengu ni kama chuo kikuu ambapo watu mbalimbali huchukua kozi tofautu tofauti na kila mmoja hupimwa kwa kozi yake|.
Na,Upweke wa mwanadamu,hapa ninamaanisha,ile hali ya mwandamu kubakia pekee,mwanafalsafa mmoja alisema kuwa every one in the world is self anda we are together when we are together ,kwa kiswahili  Kila mtu ulimwenguni yu pekee na tuko pamoja tunapokuwa pamoja
Tumekuwa tukikutana na watu wengi mashuleni,safarini,kazini,na kwingineko ,hata hivyo muda unapofika tumekuwa tukiwaacha marafiki zeku na kuishi mbali nao.Ingawa wakati mwingine tunatamani tusitengane nao lakini,muda unapofika tunatengana nao ,sote kwa pamoja tukihuzika sana na wakati mwingine kulia sana,ukisoma  matendoutaona kuwa ,wale wazee walihuzunika sana kwa vile Paulo alivyowaaga na kuwaambia hawatamwona tena uso.Wapo wengine husema kuwa hawezi kuwa mbali na wazazi wao na wengine na wapenzi wao.
 Hata hivyo ndoto zao zimekuwa zikizimika pale,wale wawapendao wanapokuwa mbali nao kwa kufariki au kwenda kuishi mbali nao ,huenda kimasomo,ndoa na kikazi.
Siku moja ,nikiwa kazini kwetu ,tuliletewa taarifa ya kuhamishwa lindoni wafanya kazi wenzetu,askari mmoja alipopata hizo taarifa alionekana kuhuzunika sana na nikamsikia akijiuliza swalisijui itakuwaje tu? Kwanini imekuwa hivyo?Aah! tuliwazoea sana,tutabaki wapweke mno.
 Lakini hata sisi pia tumekuwa tukijiuliza maswali kama hayo wakati watu tunao wapenda wanapotuacha na kuwa mbali nasi.Maisha yetu ya shule tumekutana na kuzoeana na watu wengi,lakini baada ya kumaliza shule wengi wa marafiki zetu tumewapoteza,hatuwaoni tena.Lakini hata tukikutana napo kila mmoja wetu huwa  amebanwa na kazi na masomo,hivyo tunatamani tuongee na kukaa pamoja kama awali lakini kazi na masomo yametubana,kila mmoja aliko.
Lakini nimefundishwa jambo fulani kwa kusoma dondoo moja inayosema kuwa watu wanaotuzunguka wapo kwa ajiri ya kutuwezesha na sisi kuwawezesha kutimiza kusudi fulani katika sehemu fulani.Ndiyo maana mtu mwingine alisema every where in the world is full of friends and relatives,yaani kila mahali ulimwnguni pamejaa marafiki na ndugu
Tunaweza kujiuliza ,kwanini tunapokuwa marafiki tukaenda sehemu  fulani mbali na nyumbani tukifika huko,kila mmoja atajikuta amepata rafiki yake? Au kwanini una rafiki huyo uliye naye na si mwingine?Kila tunakoenda tumekuwa tukikutana na marafiki ambao tumeshirikiana nao kutimiza kusudi lilotupeleka mahali hapo.
Nilipomaliza kidato cha nne nilihizunika sana  kwasababu nilienda kuishi mbali na marafiki zangu ,tulikuwa tumezoeana sana,na tumeshirikiana katika kufanya mambo mengi,niliamini kuwa sitapata marafiki kama wale.Hata hivyo nilivyojiunga na kidato cha tano,siku chache sana nilijikuta nimepata marafiki ambao nao tulipedana sana.Hata hivyo baada ya kumaliza kidato cha sita niliwapoteza tena hao rafiki zangu,nikahuzunika sana.
Hii hali ilikuja ikaniathiri sana nilipokuja kujiunga na chuo,kwani nilionekana kujitenga sana na wanachuo wengine nikichagua marafiki wachache sana nitakaoshirikiana nao kimasomo,pindi niwapo chuoni.Hii ni kwasababu ninaamini kuwa, watu wote hao,wanapita,muda mchache ,baada ya kumaliza chuo nitaachana nao kama rafiki yangu mmoja aliuvyozoea kusema kuwa we are here for seasonyaani tuko hapa kwa msimu.
Kwa hiyo kikubwa nilichokuwa ninakiangalia nikutimiza kusudi langu lililonipeleka pale,ndiyo maana nikatafuta marafiki nitakaoshirikiana nao,kutimiza hilo kusudi.
Kuna watu wanaogopa kuandamana  na Kristo kwasababu ya hofu ya kutengwa na wazazi wao au familia yao.Lakini Yesu alisema tukiwapenda wazazi wetu zaidi ya yeye hatutakuwa  tunamfaa(Mathayo 10:37).tunajisahau kuwa kila mtu atasimama peke yake mbele za kiti cha hukumu na pia kila mtu duniani anaondoka duniani kwa wakati wake.Hata kama mkifa siku moja lakini bado kabri litawatenganisha.Kwa hiyo ndugu zangu tusiogope kumfuata Yesu kwasababu ya kuogopa kutengwa na familia  zetu,tunapaswa kujua kuwa ,kila mtu atasimama pekee yake mbele za kiti cha hukumu.
            Tunaweza kujiuliza swali kuwa tunashindaniaje sasa ufalme wa mbinguni? Kama tulivyoona kuwa shidailiyomfanya mwanadamu aondolewe katika bustani ni kukataa kutii agizo la Mungu,nah ii ilisababishwa na ulaghai wa shetani,kwahiyo mashindano yalipo sasa hivi ni yale ya kufuata sheria na kanuni za Mungu ambazo ameagiza tuzifuate.
Kanuni ya kwanza kabisa ni ,kumwamini Kristo,kutubu dhambi,kubatizwa na kujazwa roho Mtakatifu(yoh 3:16-18,Mark 16:16).Kanuni inayofuata ni kuishi maisha matakatifu(Ebr 12:14,1pet 1:13-16).
            Kwahiyo kila mtu anapaswa kukaza bidii kwa kuyafuata yale Mungu alyomwamuru kufuata na kuyakataa yale ambayo shetani anamwamuru kuyafanya.Kwahiyo ushindani  ulipo hapa ni ,kumtii Mungu au kumtii shetani?
  Jiulize je ni shetani au ni Mungu unayemfuata? Ukifuata anachokisema Mungu utaishi naye milele na milele,na ukifuata anachokisema shetani ,utaadhibiwa naye katika ziwa la moto.