HIRIZI YA MAPENZI SEHEMU YA 3
*SEHEMU YA TATU*
★★★★★★★★★★★★★★★
Nilimpa ishara rafiki yangu, nikaingia ndani na kufunga mlango.
“Huyu rafiki yangu ana matatizo kidogo ameniomba nikamsaidie, naomba dakika tano tu nitarudi my”. Nilimdanganya Jacq huku nikiwa navaa nguo zangu harakaharaka.
“Najua unachotaka kukifanya Jay, lakini mimi nitafanya zaidi ya hivyo, wewe jaribu tu kunikimbia, kesi itakua kubwa zaidi kwako kuliko unavyofikiria”. Jacq alisema kwa kujiamini huku akionesha kukerwa na kitendo changu cha kutaka kuondoka mle ndani.
“Ina maana hunielewi au vipi? Kwahiyo nisimsaidie rafiki yangu katika tatizo lake?” Nilimhoji Jacq.
“Acha ujinga Jay, unahisi sijui unachokifanya? Najua sana”. Jacq alionekana kuamini katika hisia zake. Nikamuangalia sana kwa makini, nikaona amemaanisha kitu kutoka moyoni. Hapa nilikua nimeshamalizia kuvaa hadi 'Cap' yangu nyekundu, na raba zangu nyeupe, tayari kwa kutoka. Nikamtizama kwa makini sana kiasi cha dakika moja, kisha nikaugeukia mlango na kutokomea. ★★★★★★★★★★★★★★★
*HIRIZI YA MAHABA* Iliyokulika zaidi kwa jina la Ndere au Kindere, ndiyo iliyokuwa 'ikiniweka mjini' kwa kipindi hiki. Niliringia sana hirizi hii, kwa sababu ilinikutanisha na wanawake wengi wa aina tofauti. Hakuna mwanamke ambaye angeweza kuniringia kwa wakati huu. Kila mwanamke niliyemtaka niliweza kumpata.
Kwa muda wa miaka mitatu tu tangu nimiliki hirizi hii, nilishatembea na wanawake wasiopungua mia moja na sabini. Walikuwemo wake za watu, wachumba za watu, wanafunzi, walimu, wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi, maaskari, madakari, manesi, wauguzi, maafisa elimu mpaka wafanyabiashara.
Sikuwa najali sana kuhusu magonjwa na kitu kingine chochote, na wala sikuchukua tahadhari yoyote katika kufanya ngono zote ambazo nimezifanya. Nilihisi kawaida sana, nilijali starehe zaidi.
Kwakweli kwa muda huu tangu nimiliki hirizi hii, karanga nauza kwa kutafuta tu wanawake warembo wa kila idara, na si kwa ajili ya pesa, kwani nilikuwa na wanawake wengi waliokuwa wakinihudumia. Sikujutia hata kidogo pesa yangu niliyoipata kwa tabu kwenda kuitoa kununulia mbuzi ambaye damu yake ndiyo iliyotumika kutengenezea hirizi hii. Kwa sasa nilihisi faraja sana.
Nilivaa na kula nilichojisikia kupitia hirizi hii. Wanawake wote warembo walikuwa wa kwangu.
Wengi wa wanawake walinitaka nihamie kwao kutokana na mazingira mabovu niliyokuwa naishi pale uswahilini, lakini nilikataa kufanya hivyo. Na hii si kwa sababu nyingine, bali lilikuwa moja ya sharti la hirizi hii.
“Usihamie kwa mwanamke hata kama umeshawishika kiasi gani, utapoteza ufalme wako”. Bado yaliendelea kunijia kichwani maneno haya ya mganga wangu.
Sikuwa na namna zaidi ya kuendelea kuishi pale. Maisha yangu yalikuwa ya namna hii, kubadilisha wanawake kila leo. Sikujua nitaishia wapi, lakini kama wasemavyo *'Ujana maji ya moto'*, sikujali sana hali ya baadae.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Nilimwacha Jacq pale kitandani akiwa haamini kama nimeondoka, hakutegemea.
Nikatoka nje ambapo Nira alikuwa akinisubiri, tukaongozana na kutembea kuelekea kwake.
Tukatembea hatua chache sana, kwa mbali nikaona mtu ambaye nilihisi namfahamu akiwa anatembea kuja huku tunakotokea sisi. Kwahiyo tukawa tunatembea kuelekeana. Kadri tulivyozidi kumkaribia ndivyo nilivyojihakikishia kuwa ni yeye huyu ninayemfahamu mimi.
Tukatembea mpaka tukawa tumemfikia kabisa, naaam ni yeye kweli.. Rahel, mke wa mtu aliyetokea kukolea kwenye penzi langu kiasi cha kumsahau mumewe ambaye wapo kwenye ndoa kwa miaka saba sasa.
“Siku ya nne leo nakupigia simu hata hupokei simu zangu, ndo nini sasa Jay?” Aliniuliza Rahel kabla hata ya salamu.
“Ndio salamu ya kwenu hiyo?” Nilimzingua.
“Ooh samahani mpenzi, nina hasira ndo maana nimekuwa hivi” Alirudi chini. Na hiki ndicho kitu kikubwa nilichompendea Rahel, alikuwa mwepesi sana wa kurudi chini anapoona amekosea, tofauti hata na Jacq na wengineo ambao mara nyingi walijiona wako sahihi.
“Simu yangu imepotea mlemle chumbani kwangu, siku ya nne leo naitafuta siioni, na ilikuwa 'silent' nikiipiga inaita lakini sijui iko wapi”. Nilidanganya.
“Ok, haina shida, nikahisi una tatizo” Aliridhika Rahel na uongo ule.
“Ndio, tatizo ninalo” Na mimi nilisema kile ambacho hakukitegemea kukisikia.
“Eeenh? Tatizo gani tena?” Aliuliza kwa kuhamaki.
“Mambo tu ya ulimwengu” Nilimjibu haya huku nikionyesha ishara ya kutaka kuendelea na safari yangu, kwani Nira alishanifinya kwa siri kuwa nifupishe maongezi tunachelewa.
“Naomba basi twende pale kwako tukaongee kidogo, nimekuja kwa ajili yako baby, afu nina zawadi yako pia leo. Na pia nataka nkuachie ile laki 3 ulosema unahitaji kwa ajili ya mambo yako”. Rahel aliongea akijaribu kunishawishi nirudi nyumbani kwangu.
“Samahani Rahel, waweza kunipa hivyo vitu vyote hapahapa, maana nina safari muhimu kidogo” Nilipitisha ombi langu nikiashiria kuwa siwezi kurudi nyumbani kwa muda huu.
“Tangu lini nikafanya hivyo? Leo iwe ya pili? Kama safari yako ni muhimu kuliko mimi na zawadi zangu unaweza kwenda, ila kwa barabarani hapana” Aliongea kwa msisitizo Rahel pasipo kujua ugumu wa jambo linalonikabili.
★★★★★★★★★★★★★★
Je, Jay atarudi nyumbani kwa ajili ya zawadi za Rahel? Au nini kitatokea..??!!
Usikose HIRIZI YA MAPENZI SEHEMU YA 04.