Kufanya Mapenzi Mara kwa Mara Kunaboresha Afya yako
June 27, 2019
Edit
Kufanya mapenzi ni mojawapo ya vitu vichache ambavyo watafiti wanasema vinamfanya mtu aburudike huku mwili wake ukifaidika kutokana na tendo hilo.
Utafiti umeonyesha kwamba kufanya tendo la ndoa mara kwa mara kunatibu mafua, kuepusha magonjwa ya moyo, kunazuia kansa na hata kuongeza urefu wa maisha.
Watafiti katika chuo kikuu cha Nottingham University nchini Uingereza wamegundua kwamba wanaume wenye umri zaidi ya miaka 50 wanaofanya tendo la ndoa mara kwa mara wana uwezekano mdogo sana wa kupata kansa ya kibofu.
Watafiti hao walikanusha madai kwamba kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara 20 kwa mwezi kunaongeza uwezekano wa kupata matatizo ya moyo.
Madaktari wamekubaliana kwamba mapenzi ni kama shughuli zingine za kawaida na ni mazoezi bora kwa afya.
“Kwa kulinganisha na mazoezi, kufanya mapenzi ni sawa na kutembea zaidi ya kilomita moja au kupanda na kushuka ngazi za majengo mawili marefu” alisema Dr Graham Jackson wa hospitali ya St Thomas.
Utafiti uliofanywa na Chuo kikuu cha Queens University cha Belfast umesema kwamba kufanya mapenzi zaidi ya mara tatu kwa wiki kunapunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo.
Tendo la ndoa pia linasaidia kulinda mifupa. Dr Sarah Brewer alisema: “kiwango cha Testosterone kimeonekana kuongezeka wakati tendo la ndoa na baada ya tendo la ndoa”.
Utafiti huo ulibainisha kwamba kwa wanaume na wanawake ili waweze kupata faida za tendo la ndoa inawabidi wafanye tendo hilo mara kwa mara.
“Itumie au ipoteze” ndiyo ushauri uliokuwa ukitolewa kwa wazee na wanasayansi toka nchini Finland.
Pamoja na faida za tendo la ndoa ,tendo hilo pia lina hasara zake kama vile kupata magonjwa ya zinaa iwapo kinga haitatumika.
Tangia kugunduliwa kwa viagra miaka 10 iliyopita idadi ya watu wenye umri zaidi ya miaka 45 walioambukizwa magonjwa ya zinaa imeongezeka maradufu.