Jinsi ya Kukabiliana na Maumivu ya kuachana na Mpenzi.
June 20, 2019
Edit
badilisha mazingira.
ni vizuri kuondoka katika mazingira yatakayokuwa yakikupa kumbukumbu kila mara juu ya yule uliyekuwa nae, jaribu kuwaepuka hata wale marafiki zake ambao wanaweza kukuuliza kuhusu yeye, hii itakufanya kupata nafuu ya maumivu yako.
jifunze kusamehe na kusahau.
ni jambo zuri kujifunza kusamehe na kukubaliana na hali halisi ya kile kilichotokea, inawezekana mliachana kwa hasira kutokana na kile alichokufanyia kwa kipindi icho, jifunze kukubali kosa na moyo wako uwe mwepesi kusamehe kile alichokukosea ili usibaki na hasira.
sitisha mawasiliano.
kuna watu wanakuwa na maumivu na wale waliowaacha lakini bado anaweza kumtafuta na hata kumpigia simu, hiyo inaongeza maumivu kwa sababu yapo utakayokumbuka kuhusu yeye, epuka kuwsiliana nae na hata akikutafuta basi tafuta njia ya kumuepuka mtu huyo.
jipende na kujithamini mwenyewe.
kisaikolojia wataalamu wanasema watu wengi wakiachwa na wapenzi wao au kugombana basi wanaanza kujishusha na kuona kuwa wao hawafai na wala sio wa thamani sana, kumbe mtu anaweza kuamua kukuumiza tu kwa sababu zao na hata bila kujali kama atakuumiza wewe, sasa huu ndio muda wa kujiona bora na kujipenda mwenyewe kuliko maelezo.Achana na fikra kwamba wewe sio bora kuliko yule aliyemfata au kumpata baada yako.
usitafute wa kuziba pengo.
mara nyingi imekuwa ni kawaida kwa watu wanapoumizwa wanakimbilia kutafuta mtu mwingine kwa ajili ya kuziba pengo ili kukwepa maumivu yale ya mwanzo, hii ni mbaya sana kwa sababu ikitokea ukaumizwa tena unapata maumivu makubwa zaidi kuliko yale ya awali.jipe muda kwanza na kisha jitafakari na jipe muda wa kuponesha makovu yako ya maumivu ya mapenzi.