HATA KAMA UMEUMIZWA SANA, BADO UNAYO NAFASI YA KUPENDA TENA - Chumba Cha Mapenzi -->

HATA KAMA UMEUMIZWA SANA, BADO UNAYO NAFASI YA KUPENDA TENA

HABARI yako msomaji wa kona hii! Ni matumaini yangu kwamba uko poa na unaen­delea na majukumu yako ya kila siku. Nakukaribisha tena jamvini ili tuzungumze na kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu uhusiano wa kimapenzi.

Leo nimeamua kuja na mada hii baada ya kusikia malalamiko kutoka kwa wa­somaji wangu kadhaa ambao wanalia kutokana na kuumizwa na wenzi wao ki­asi cha wengine kufikia hatua ya kujiapiza kwamba hawawezi tena kupenda.

Unapozungumzia suala la maumivu ya mapenzi, japokuwa huumiza sana hasa kama ulikuwa na mapenzi ya dhati na mwenzi wako na baadaye akaaamua kukugeuka, siyo suala geni hapa duniani.

Unapolia leo kwa sababu ya mapenzi, elewa kwamba ma­milioni ya watu wa­nalia kama wewe ingawa tunato­fautiana namna ya kukabiliana na maumivu. Lakini cha kujiuliza ni je, mpen­zi wako akikuumiza sana, ni sahihi kujiapi­za kwamba hutapen­da tena?

N i s a h i h i k u s e ­m a kwamba siku hizi hakuna mapenzi ya ukweli kwa sababu tu amekuumiza? Ni sahihi kusema wanaume wote wako hivyohivyo au wanawake wote ndivyo walivyo?

Ukweli ni kwamba, unapovunjika moyo haimaanishi kwamba huo ndiyo mwisho wako wa kupenda. Unapo­jiapiza kwamba hutapenda tena au hutamwamini mtu tena, ni makosa makubwa kwa sababu kama uliyekuwa naye ameshindwa kuiona thamani ya penzi lako, yupo ambaye atakuthamini na kukuheshimu.

Kuna usemi maarufu kwamba mlango mmoja unapojifunga, mwingine huwa unafunguka muda huohuo lakini wengi wetu hupoteza muda mrefu kuutazama ule uliojifunga badala ya kuufuata ule ul­iofunguka.

Msemo huo una maana kubwa kwenye mapenzi kwamba kama mwenzi wako amekutenda, amekuvunja moyo, amekusononesha na kukufanya ulie, jua kwamba hakuwa riziki yako. Huwezi kujua Mungu amekuepusha na nini kwa hiyo badala ya kujiapiza na kukufuru, ni bora ukakubaliana na ukweli, japo huwa inauma sana.

Ukishaukubali ukweli, unakuwa kwenye nafasi nzuri ya kupona maje­raha ndani ya moyo wako na nakuhak­ikishia, hata kama ulimpenda vipi huyo uliyekuwa naye, kama amefikia hatua ya kukuumiza na kuuvunja moyo wako, hakuwa riziki yako, endelea kumuomba Mungu kwa sababu yupo ambaye ndiye hasa aliyepangwa kuwa wako.

Upo usemi mwingine kwamba watu wengi huwa hawaoni umuhimu wa kitu mpaka wanapokipoteza, na wakati huo­huo huwezi kujua ulichokuwa unakikosa mpaka pale utakapokipata. Yawezekana ulimpenda sana lakini huwezi kujua ulikuwa unakosa nini mpaka utakapoku­tana na yule mwenye mapenzi ya dhati, ambaye atakuheshimu na kukutunzia penzi lako.

Kinachowaumiza wengi huwa ni ma­tarajio makubwa wanayokuwa nayo kwa wenzi wao. Unapomuonyesha mwenzi wako mapenzi ya dhati, haimaanishi kwamba na yeye atakuonyesha kama unavyotaka iwe.
Unaweza kupenda sana lakini ukaishia kulipwa mabaya, kitu cha kuzingatia ni kwamba kama umeamua kupenda, penda kwa moyo wako wote na kama unayem­penda ni sahihi kwako, utajikuta nafsi yako iki­ridhika na utakuwa na furaha.
U n a p o w e ­ka mategemeo makubwa kwamba mwenzi wako naye atakupenda ka­tika kiwango sawa na kile unachom­penda, ikitokea ameenda tofauti, maumivu yake huwa makubwa sana.