Njia bora ya kuishi na Mwanaume/Mwanamke mwenye hasira
May 07, 2019
Edit
Read More
Na kama ukifahamu hasira yako ina ishara za tatizo kubwa, utaweza kuanza kuponya hio misingi ya tatizo. ujiruhusu kukasirika lakini bila ya kujilaumu au kujijaji mwenyewe. na hii itakuweka vizuri kwa vile umeonyesha hasira yako kwa mwenza wako.
Kuwa na utulivu ni dalili za kutubadilisha tabia zetu badala ya kulaumu watu kutobadilisha tabia zao. ni chaguo lako la kubeba hasira au kujielezea ili kuondokana na hilo tatizo.
Hasira Hujenga.
Nina uhakika kuwa vyovyote vile mke au mume au rafiki mwenye hasira huwezi kufikiri kuwa hasira itakupa afya na kuwa mtu wa kuleta mazuri , lakini kuna maajabu hutokea unapotumia hio hasira kwa utulivu .
Hii sio nguvu mbaya , ni nguvu ya kujenga. tunatakiwa tu kuchagua kutumia kwa njia nzuri, na tunapofanya hivyo, tutakuja na mawazo mazuri ya kukabiliana na tatizo.
Kwa hio angalia hasira yako kwa ndani zaidi. mfano kama mwenza wako anapenda kutupa nguo kila sehemu, na wewe hilo linakuudhi , ni vizuri kukaa na kumweleza kuwa anaweza kufanya kitu unachotaka afanye. Kuna wengine wengine sijui wakoje wakienda chooni hawaflash. na kila siku mke akienda kusafisha anakuta uchafu . na kitendo hicho kinampa hasira . hivi vitu ni vya kurekebishana kama ukikaa kwa utulivu na kufikiria jinsi ya kuongea nae.
Unaweza kufikiria huo mfano ni rahisi , lakini kitu kikubwa ni kwamba tunahitaji kujifunza jinsi ya kupata solution ndogo ndogo kwanza, hio ndio njia ya kuweza kushughulikia tatizo kubwa la hasira. na utakuwa na nguvu ya kulithibiti tatizo la hasira.
Jinsi Ya Kuwa Mke Au Mume Mwenye Hasira.
Kabla ya kuonyesha hasira, ni muhimu kwanza kuondoa woga, woga wa kukataliwa na kutokueleweka, na ukumbuke woga ni halali na upo kwa sababu.. Lakini kuwa tayari kuonyesha hasira ya upande mwingine ni iwe dalili nzuri ya uaminifu. unaamini kwamba mahusiano yenu yanasimamia ukweli na uaminifu.
Kwanza kabisa unaweza kujitenga na hasira yako kwa kusema hivi vitu, Najisikia hasira kuhusu hiki kitu na hapo lazima useme kwa nini.” Kitu kingine unaweza kuandaa kuwajibika kwa hisia zako na kuingia kwa nia ya kuleta badiliko zuri.. na mwisho ni kuongea na mwenza wako kwa lugha nzuri ya kueleweka, inayowezekana, itakusaidia usijilaumu wala kulaumiwa na mtakuwa na maongezi mazuri.
Kubadili mpangilio wa akili yako kuhusu hasira na kutumia kwa faida yako, utaleta Amani ya kutosha,mawasiliano mazuri na kuongeza urafiki wa kimapenzi nyumbani kwako.
Nitajitahidi mazoezi haya kila mara na kujitahidi kutafakari kila siku ili ninaposikia hasira niitulize na kuwa na maamuzi mazuri kwenye mahusiano yangu.