SABABU ZA WANAUME KUTOKUWA WAAMINIFU - Chumba Cha Mapenzi -->

SABABU ZA WANAUME KUTOKUWA WAAMINIFU


1. Utupu au upweke ndani ya moyo wa mwanaume
Pamoja na kwamba wanaume huonekana wakiwa jasiri sana kwa nje ila ieleweke kwamba ni viumbe dhaifu ndani, ni viumbe wasioweza kuvumilia upweke ndani yao, wakati wote hutamani kuwa karibu na mwanamke hata kama akiwepo karibu hawaelewani mara kwa mara.
2. Uasili wa kiu kubwa ya mwanaume katika tendo la ndoa
Kiasili na kibaiolojia mwanaume anakiu kubwa na utayari wa kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, mwanaume wa kawaida anaweza kutamani kufanya tendo la ndoa hata kila siku, na wengine hata marambili kwa siku kama kila kitu akilini na katika afya yake ni sawa. Utayari na uwezo huu ni tofauti sana kulinganisha na wanawake ambao kama akifanya tendo zuri la ndoa na hamu yake ikitoshelezwa basi anaweza kukaa muda fulani bila kutamani tena.
3. Kubadilika kwa uzuri, urembo na maumbile ya mke
Mara nyingi ninapoongea na wanawake huwa ninawaambia kwamba mume wako anakupenda uwe vile alivyokupenda alipokutana nawewe, mabadiliko yoyote ya ziada kutoka kwenye ile hali iliyompa hamasa awali yanaweza kuigharimu ndoa yako. Wanaume ni watu wenye kuhamaki au kuwa makini kwenye umbo, umbile na muonekano wa mpenzi wake kwasababu kwa asili mwanaume huvutiwa zaidi na akionacho, mwanaume hufungulia milango ya hisia inayohusu tendo la ndoa kupitia anachokiona zaidi kuliko vitu vingine vyote