JINSI YA KUMTAMBUA MWANAUME TAPELI WA MAPENZI - Chumba Cha Mapenzi -->

JINSI YA KUMTAMBUA MWANAUME TAPELI WA MAPENZI


UTAMJUAJE MWANAUME TAPELI?
Licha ya kuwa na mbinu nyingi za udanganyifu lakini tapeli wa mapenzi unaweza kumbaini kuanzia hatua za awali pindi anapoanza kukuwekamikononi mwake. Msome anakuja kwa gia gani? Yawezekana akakuambia kuwa atakuoa lakini hilo usilitilie maana haraka; wewe weka akiba ya kumpenda.
Endelea kumfuatilia taratibu mwenendo yake. Angalia nafasi anayokupatia na jinsi anavyoheshimu hisia zako. Angalia papara zake katika kutekeleza matamanio ya mwili, utambaini tu kwamba anachokitaka kwako ni tendo tu na baada ya hapo hatokuhitaji tena. Usimpende mwanaume wa aina hiyo. Jipe muda wa kumchunguza. Muweke karibu ili upate
kumwelewa zaidi, mathalan waweza jenga desturi ya kukaa naye mara kwa mara huku nia yako ikiwa ni kumsoma zaidi mazungumzo yake, tabia na maisha yake kwa jumla. Mchunguze ujue je ni kweli ana nia ya dhati ya kuwa na wewe? Safari yake ya nyuma ikoje? Kwako ana matarajio gani? Nasisitiza usimpende katika hatua hizi, muweke karibu.
Tapeli huwa hawezi kuvumilia muda mrefu, hawezi kukuficha muda mrefu. Atataka mjuane, mmalizane haraka. Mwenye mapenzi ya dhati, atatengeneza mazingira ya urafiki mzito (strong relationship). Atajikita katika kukuweka karibu na marafiki zake, ndugu zake na hata wazazi wake.