Jinsi ya kujua jinsia (gender) ya mtoto tumboni bila ultrasound
June 16, 2019
Edit
Leo nimetafakari na kuamua kuandika uzi wa kuhusu maswala muhimu kidogo kwa wanandoa/wanao tegemea kupata mtoto.
Jambo moja wapo ambao linatia furaha katika maisha ya wazazi/wapenzi ni pale wanapo tegemea mtoto. Mambo chungu nzima hua yanatia hamasa na ushawishi kuhusiana na huyo mtoto, kuanzia jinsia yake kama ni wa kiume au kike na kadhalika. Maandalizi huanza kufanywa kabla hata ya mtoto kuzaliwa, hii ikijumuisha manunuzi ya vitu kwaajili ya mtoto na majina pindi atakapo zaliwa.
Madaktari wana uwezo wa kujua jinsia ya mtoto ambae hajazaliwa wakati wa ULTRASOUND hospitalini. Na wachache hawatambui ya kua mtoto anaweza akahisiwa jinsia yake kutokana na dalili ambazo mama mjamzito huzipata, kuanzia mabadiliko ya kimwili, kulala na mpaka upendo wa vyakula fulani.
Utastaajabu kujua kuna uwezekano wa viashiria kuhusiana na jinsia ya mtoto anaetegemewa, bila kwenda hospitali na kutumia ULTRASOUND.
Kuna dalili nyingi ambazo sinaweza kukupa taarifa kuhusiana na jinsia ya mtoto kabla ya kuzaliwa. Kutokana na utafiti, ume baini haya yafutayo kama viashiria vya kujua jinsia ya mtoto kabla hata hajazaliwa;
18) Umachachari wa mjamzito (Clumsiness).
Kwa kila jinsi mwili/tumbo la mjamzito linavyokua, umachachari hua haukosekani, ila unapopitiliza mipaka kuliko kawaida, basi kuna uwezekano mkubwa wa kujifungua mtoto mwenye jinsia ya KIUME.
17) Kukua kwa Maziwa/Matiti (Breast Size).
Katika kila hatua ya mimba, mwanamke hua anagundua ni jinsi gani maziwa/matiti yake hubadilika kwa kukua. Kama ziwa/titi lake la kulia likitokea kuwa kubwa kuliko la kushoto, basi kuna uwezekano mkubwa wa kujifungua mtoto wa KIUME. Na kama titi/ziwa la kushto likiwa kubwa kuliko la kulia, basi kuna uwezekano mkubwa wa kujifungua mtoto wa KIKE.
16) Rangi ya Chuchu (Nipple Color).
Rangi ya chuchu kipindi cha ujauzito zinaweza kuashiri jinsia ya mtoto, rangi inapokua ya kiza (darker) kuliko kawaida ni dalili ya kujifungua mtoto wa KIUME, na kama rangi haijabadilika katika hatua za mimba ni dalili ya mtoto wa KIKE.
15) Aina ya Ulalaji (Sleeping Position).
Kupendelea kulalia ubavu wa kulia ni dalili za kujifungua mtoto wa KIUME, na kupendelea kulalia ubavu wa kushoto ni dalili ya kujifungua mtoto wa KIKE.
14) Kuumwa Kichwa (Headache).
Kama mjamzito atakua na matatizo ya kuumwa kichwa mara kwa mara, mtoto wa KIUME yupo njiani kuja. Na kama hatokua na matatizo ya kichwa, basi uwezekano wa mtoto wa KIKE kuzaliwa.
13) Uzito wa Baba (Dad’s Weight).
Kama mzazi wa kiume akiongezeka kilo, ni dalili za mama mjamzito kujifungua mtoto wa KIKE, na kama mzazi wa kiume asipo ongezeka kilo/au kupungua kilo ni dalili za mtoto wa KIUME.
12) Tumbo la Uzazi Kua Juu au Chini (Carrying High or Low).
Kama tumbo la mjamzito litakua juu, ni dalili za kuzaliwa mtoto wa KIKE, na kama tumbo la uzazi litakua chini basi inaashiria mtoto wa KIUME.
11) Tamaa ya Chakula (Food Craving).
Tamaa ya kupendelea vyakula vya chumvi/ukali basi ni dalili ya kupata mtoto wa KIUME, na kupendelea kula vyakula vya sukari ni dalili ya mtoto wa KIKE.
10) Miguu Kuvimba (Foot Swelling).
Kama miguu ya mjamzito haivimbi, basi inaashiria mtoto wa KIKE, kwani mtoto wa KIUME ana uwezo wa kumwongezea mjamzito uvimbaji wa miguu, mara mbili ya size ya huyo mjamzito miguu yake.
9) Joto la Nyayo za Miguu (Foot Temperature).
Kama nyayo za miguu zitakua za baridi, kuna dalili ya kujifungua mtoto wa KIUME, na kama nyayo hazijabadilika joto lake halisia ni dalili za mtoto wa KIKE.
8) Kugawanyika Kwa Uzito Mwilini (Weight Distribution).
Kama mjamzito ataongezeka kilo/uzito mwili mzima, ni dalili za kujifungua mtoto wa KIKE. Na kama ataongezeka uzito kwenye tumbo tu ni dalili za mtoto wa KIUME kuwa njiani.
7) Nywele za Mwilini (Body Hair).
Nywele za mwilini kukua kwa haraka na kua imara, ni dalili za mtoto wa KIUME kuzaliwa, wakati dalili za mtoto wa KIKE hua nywele hazioti mwilini.
6) Unawiri wa Nywele Kichwani (Hair Texture).
Nywele nzito na zenye mafuta/kunawiri ni kiashiro cha kujifungua mtoto wa KIUME, na nywele kavu/kukatika/kukosa mvuto/rough ni dalili ya kujifugua mtoto wa KIKE.
5) Kipimo Cha BAKING-SODA (The Baking Soda Test).
Chukua vijiko viwili vya baking soda na kisha changanya na mkojo wa mjamzito, kama baking soda itatoa mapovu ya gas na mliokama wa kuchemka (fizzes), ni mtoto wa KIUME anakuja. Kinyume na hapo basi atakua wa KIKE.
4) Mstari Tumboni (Linea Nigra).
Huu ni msitari ambao hutokea katika tumbo la mjamzito, mstari huu ukitokea na kuishia chini ya kitovu, basi inaashiria ujio wa mtoto wa KIKE, na kama ukipitiliza mpaka juu ya kitovu, ni kiashirio cha kuja kwa mtoto wa KIUME.
3) Furaha/Muwako/Kunawiri Usoni (The Glow).
Ni mtoto wa KIUME pekee ndio ambae humpa muwako/sura ya furaha/kunawiri kwa uso wa mama mjamzito. Mtoto wa kike humchosha sura mama yake muda wote.
2) Chunusi (Acne).
Kubeba mimba ya mtoto wa KIKE huwaletea wajawazito chunusi usoni, ni dalili moja wapo. Vinginevyo, atakua mtoto wa KIUME.
1) Mabadiliko Ya Ngozi (Skin Changes).
Kama ngozi ya mjamzito ikibadilika na kua yenye mafuta (oily skin) ni dalili za kuashiria mtoto ajae ni wa KIKE, na kama ngozi ikibakia kua kavu (dry skin) ni dalili za ujio wa mtoto wa KIUME.