Aina za wanawake lazima waachwe na waume zao - Chumba Cha Mapenzi -->

Aina za wanawake lazima waachwe na waume zao

                                                                               
  1. MWANAMKE MWENYE KUTUMIA MABAVU:
Wanaume hawapendi aina hii ya mwanamke. Kimaumbile mwanaume anapenda awe mwenye maamuzi anayeilinda na kutetea familia yake, jambo ambalo haliendani na silika ya mwanamke mwenye mabavu ambaye hawezi kubadilika na mwenye kupenda udhibiti endelevu, jambo ambalo humsukuma mwanaume kutafuta mwanamke mbadala ambaye anatamani awe chini yake.
2.MWANAMKE AMBAYE HASHIRIKIANI NAYE KATIKA YALE ANAYOYAPENDA:
Mwanaume anapooa anaweza asifikirie kuyaacha mambo anayoyapenda, kwa sababu hapendi kuhisi kana kwamba yuko jela. Na iwapo mkewe hatoshirikiana naye katika mambo hayo, anaweza kutafuta mwanamke mwingine ambaye anamjali na kushikiana naye mambo anayoyapenda.
3.MWANAMKE ASIYEPENDA WATOTO:
Watoto ni kitulizo cha macho na moyo wa mke na mume. Mwanamke asiyependa watoto kuna uwezekano mkubwa kwa mume kutafuta mwanamke mwingine. Hapa mwanamke ninayemkusudia ni yule asiyependa kuzaa au asiyewajali watoto.
4.MWANAMKE ASIYEKUWA MWELEWA NA MKOSEFU WA BUSARA:
Mwanaume anampenda mwanamke mpole, mwenye soni na mwenye adabu, lakini hampendi mwanamke aliyezubaa na asiyekuwa na uelewa na mkosefu wa busara. Hata akimuoa atamchoka na kutafuta njia mbadala. Licha ya mwanaume kutompenda mwanamke mwenye mabavu lakini hapendi ahisi kuwa anaishi na mwanamke aliyezubaa na asiyekuwa na viwango vya werevu unaochangamsha mambo katika maisha yao.
5.MWANAMKE ASIYEJALI:
Mwanaume humtafuta mwanamke ambaye atamjali yeye na watoto wake. Mwanamke anayemuenzi na kumpa nguvu katika nyakati ngumu. Hivyo, akimuoa mwanamke asiyejali, ndoa hiyo haitakuwa na mafanikio, jambo litakalomfanya atafute mwanamke wa pili atakayejaza ombwe hilo. Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume anayachukia ni kuhisi kuwa hana umuhimu wala thamani yoyote.