Utundu wa Mapenzi Kitandani una faida gani? - Chumba Cha Mapenzi -->

Utundu wa Mapenzi Kitandani una faida gani?


WAPO wanaojuta kupenda lakini mbaya zaidi wapo wanaolia kwa sababu ya vitu vidogo vidogo ambavyo vimekuwa haviwaendei sawa katika uhusiano wao. Ni jambo lililo wazi kwamba, usaliti umekuwa ukiwatesa wengi tena ukijaribu kuchunguza sababu za baadhi ya watu kuwasaliti wapenzi wao, kutoyajua mapenzi yale ya faragha ni moja wapo.Wapo wasichana au niseme wanawake ambao kimaumbile wana mvuto sana. Wamejaaliwa uzuri wa sura na kila kitu kiasi cha kutamaniwa na kila mwanaume wanayekutana naye.
Lakini linapozungumziwa suala la mapenzi kwa mwanamke, wanaume wanaangalia vitu vingi, achilia mbali hilo la muonenako, pia wanaangalia utundu na ubunifu wa faragha. Hapo ndipo panapowakosesha raha baadhi ya wanawake wazuri.
Wanakuwa ni wenye kupata bahati ya kupendwa lakini hao hao ndiyo wale ambao kila siku wanaachwa. Si jambo la ajabu huko mtaani kukutana na msichana mkali ile mbaya lakini akawa si mtu wa kutulia na mwanaume kwa muda mrefu, kwanini? Kwa sababu hayajui mapenzi.