WADADA/WANAWAKE MTANISAMEHE KIDOGO KWA HILI - Chumba Cha Mapenzi -->

WADADA/WANAWAKE MTANISAMEHE KIDOGO KWA HILI




Simkashifu mtu ila ni ujumbe tu,,pia amepata kusema mdau wa maswala ya wanawake (lu-patie)"wanaume wengi hawajafikia ndoto zao,,wanatamani wapate wanawake wa kuwatia moyo ili wafikie ndoto zao"
Ukweli mchungu ni kwamba wanawake wengi hawataki wanaume ambao bado wapo safarini kuelekea ndoto zao,,wanataka waliokwisha fika,,na bahati mbaya wako occupied,, linalotokea ni nini?wanawake wanadhani wana bahati mbaya,,unaweza ukawa unalalamika una mkosi wa kuolewa yaani kila mwanaume anakuja na ahadi nzuri,lakini baadae anakuacha,,lakini upande mwingine maamuzi yako ndiyo maumivu yako,,,kweli huenda wewe ni mtoto wa kike,,mzuri wa sura na hata umbo lakini umenyimwa hekima,,
Unampaparikia kijana mtanashati kisa ana gari na pesa,,unamwona kijana anayeenda kumbi za starehe usiku ndio mjanja,,anaevaa suruali chini ya makalio ndo sahihi kwako,,lakini yule anayeenda kwenye ibada ijumaa au jumapili unamwona mruga ruga tu a.k.a mshamba
Unampuuza na kumdharau mtu eti kisa tu kasoma lakini hana ajira,,ama kijana ambae kipato chake ni laki 2 kwa mwezi,,badala yake unamkumbatia mtu ambae ni baba fulani au ni mume wake mtu kisa tu anapesa na shida zako anakutatulia,,
SWALI;Utaolewa vipi wakati mpaka sasa unapenda kutoka na waume za watu au vijana wenye magari ya mkopo au kijana yeyote ambaye unajua huna future nae,,au ndo unamplease ili asiache kukupa pesa,,nani atakaye kuoa wewe wakati vijana wanaotafuta mke unawasema vibaya kuwa hawana hadhi ya kutembea na wewe kisa hawana misuli ya uchumi kwa muda huu,,
Funguo ya ndoa utaipata wapi wakati hapo ulipo unamnunia mke wa mtu kisa unatoka na mume wake,,DADA maisha yanabadilika mpiga debe wa leo unaweza mbadilisha akawa mwendesha gari kisha akamiliki gari yake,,hakuna mtu aliyezaliwa masikini ndo maana juhudi zinahitajika
Weka malengo mbele lini unatamani kuwa na ndoa na umri gani uzae kuliko anasa