NENO ASANTE LINA MAANA NA NGUVU KUBWA SANA KWENYE NDOA AU MAHUSIANO - Chumba Cha Mapenzi -->

NENO ASANTE LINA MAANA NA NGUVU KUBWA SANA KWENYE NDOA AU MAHUSIANO




Kinachoshangaza ni pale mchepuko anapozawadiwa kitu fulani cha thamani ya shilingi 15000,,,halafu anashukuru na kumuenzi huyo mwanaume utafikiri kapewa milioni,,,atashukuru kwa maneno,,kwa meseji ya kawaida,,kwa WhatsApp,,kwa emoji na kwa matendo,,,,sasa mke wake mtu anapewa laki tatu na anashukulia poa,,anaona yeye si ndo anastahili,,ashukuru nini sasa wakati pesa ya mumewe,,tena Bado anaona hiyo ni kidogo alistahili kubwa zaidi,,haonyeshi shukrani kwa sura,sauti hata kitendo,,,anamwangalia mumewe juu mpaka chini kwa jicho la dharau,,huku moyoni akisema"mwanaume bahili huyu"usiku baba wa watu analala kitanda kimoja na mama watoto wake,,lakini akilini anamuota yule kidumu aliyemshukuru na kumnyenyekea kama mfalme,,na asubuhi akiamka safari kituo cha kwanza kwake,,,ngoja nikwambie kitu wengine mnalalamikaga mnaibiwa waume zenu lakini ukweli ni kwamba hamjaibiwa,,mmewa sendoff wenyewe,,halafu wakipokelewa kwa mioyo mikunjufu,,mnaanza kutoa povu,,wewe endelea na hiyo TABIA,,utakuja kufahamu kwanini limao linagandisha maziwa haraka.