HAYA HAPA MADHARA KWA WANAUME YA KUTOFANYA MAPENZI MARA KWA MARA
May 14, 2019
Edit
Utafiti ulioonesha wanaume wasiofanya kitendo cha kujamiana mara kwa mara walikuwa na hatari zaidi ya kupata saratani ya tezi dume
KATIKA hali ya kawaida imeelezwa kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala la ngono kupita kiasi kunaweza kusababisha matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoiendekeza.
Mtu anaweza kuwa na mwenzi na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu hakuna kizuizi na ana haki ya kufanya hivyo.
Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande mmoja, lakini pia baya kwa upande mwingine kwa vile linaweza leta athari fulani kiafya na katika uhusiano baina ya wenzi.
Chunguzi zinaonesha miongoni mwa watu wengi wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka kwa wale wanaoiendekeza sana ngono.
Lakini pia ukiachana na athari chanya au hasi ambazo zinajulikana kwa miaka mingi miongoni mwa watu na au wataalamu, kuna nyingine ambayo haikuwa ikifahamika kwa wengi.
Inahusu utafiti mpya mpya nchini Marekani ulioonesha kuwa wanaume wanaokojoa katika tendo la ndoa mara kwa mara wana uwezekano mdogo wa
kupata saratani ya tezi dume kuliko wale ambao hawakojoi mara kwa mara.
Ikumbukwe saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na kansa kwa wanaume duniani.
Pia ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea.
Hata hivyo, satarani ya tezi dume kwa sasa inawapata sana wanaume kuanzia miaka 25.
Tukirudi katika utafiti, wanasayansi waliwafuatilia wanaume 32,000 kuanzia mwaka 1992 wakati walipokuwa katika umri wao wa miaka ya 20 na kuendelea hadi mwaka 2010.
Wakati wa kipindi hicho karibu wanaume 4,000 miongoni mwao waligundulika dalili za saratani ya tezi dume.
Wanaume, ambao walikojoa angalau mara 21 kwa mwezi katika umri wao wa miaka ya 20 walikuwa uwezekano mdogo wa asilimia 19 wa kupata saratani ya tezi dume kuliko wale waliokojoa chini ya mara saba kwa mwezi, utafiti huo ulibainisha.
Wanaume ambao walikojoa mara kwa mara katika umri wao wa miaka ya 40 walikuwa na uwezekano wa chini ya asilimia 22 ya kupata saratani ya tezi dume.
Wanaokojoa mara chache kuanzia sifuri hadi mara tatu kwa mwezi walikuwa na uwezekano wa kuwa na matatizo mengine ya kiafya na kifo cha mapema kutokana na sababu nyingine zaidi ya saratani ya tezi dume,” alisema mwandishi kiongozi wa utafti huo Jennifer Rider, ambaye alifanya uchambuzi wakati akifanya kazi katika Shule ya Afya ya Umma ya Harvard T.H. mjini Boston, Marekani.
“Wakati ugunduzi wetu ukipaswa kuthibitishwa katika tafiti ambazo zinatathimini uwezekano wa taratibu za kibailojia zinazosababisha uhusiano uliobainishwa, matokeo ya utafiti wetu yanaonesha kwamba kukojoa na ngono salama kipindi chote cha utu uzima kunaweza kuwa mkakati wenye manufaa wa kupunguza hatari ya saratani ya tezi dume,” Rider, ambaye kwa sasa yu Chuo Kikuu cha Boston, aliongeza kwa njia ya barua pepe.
Saratani ya tezi dume huchangia asilimia 15 ya kesi zote za ugunduzi wa ugonjwa huo duniani, watafiti waligusia katika Jarida Mfumo wa Mkojo Ulaya (European Urology).
Visababishi vya hatari kama vile umri, utaifa na historia ya familia ‘hazibadiliki’ waliongeza na kwamba kuna staili chache za maisha zinazoweza kutumiwa na wanaume ili kupunguza hatari.
Ili kufahamu uhusiano baina ya kukojoa mara kwa mara na saratani, Rider na wenzake walipitia takwimu kutoka maswali yaliyokamilishwa na wanaume kuhusu afya ya uzazi na kuchunguza rekodi za kitabibu pamoja na majaribio ya kimaabara kuangalia washiriki waliogundulika kuwa na uvimbe wa saratani ya tezi dume.
Wakati wa kipindi cha utafiti, kulikuwa na kesi 192 za saratani ya tezi dume miongoni mwa wanaume wanaomwaga mbegu za kiume chini ya mara tatu kwa mwezi.
Kulikuwa na kesi 1,041 kwa wanaokojoa mara nne hadi saba kwa mwezi na kesi 1,509 za wanaokojoa mara nane hadi 12 kwa mwezi, na wengine kesi 807 wanaokojoa mara 13 hadi 20 kwa mwezi na kesi 290 kwa wanaokojoa mara 21 kwa mwezi.
Moja ya changamoto ya utafiti ni kwamba iliegemea kwa wanaume walioripoti kwa usahihi na kiwango walichokojoa, watafiti wanasema.
Utafiti pia ulihusisha zaidi wazungu na hivyo kuwapo uwezekano wa matokeo tofauti iwapo ingehusisha rangi nyingine kwa kuzingatia kuwa inafahamika maradhi haya huwakumba zaidi watu weusi.
Udhahiri wa uwapo wa matokeo chanya kwa wanaokojoa mara kwa mara ulionekana zaidi kupunguza idadi ya walio hatarini kugundulika saratani ya tezi dume, waandishi wa utafiti huo wanasema.
Uhusiano baina ya kukojoa mara kwa mara na saratani ni mkubwa kwa wanaume wasio na dalili za uvimbe wa saratani ya tezi dume kama vile maumivu au matatizo ya njia ya mkojo ambao tayari wameonekana kuwa na kiwango cha chini cha uwezekano wa kugundulika na ugonjwa huo, anasema alisema Dk. Behfar Ehdaie, mtaalamu wa mfumo wa mkojo katika Kituo cha Saratani cha Kumbukumbu ya Sloan Kettering mjini New York, Marekani ambaye hakuhusika na utafiti huo.
“Iwapo kukojoa mara kwa mara kwa kweli ni kisababishi cha msingi cha saratani ya tezi dume, tunatarajia kutafiti uhusiano wa maeneo yote yanayosababisha hatari ya saratani ya tezi dume,” Ehdaie alisema kwa njia ya barua pepe.
Pia ni mapema mno kuchukulia uzito kiwango cha tendo la kujamiana kama silaha ya kuzuia saratani, alisema Siobhan Sutcliffe, mtafiti wa saratani katika Shule ya Tiba, Chuo Kikuu cha Washington huko St. Louis ambaye pia hakuhusika na utafiti huo.
“Ushiriki wa kujamiana unaweza kuwa na athari mbaya kiafya, kama vile kupata maradhi ya kuambukiza kwa njia ya kujamiana,” Sutcliffe aligusia kwa njia ya barua pepe.
dv2014035 Kukojoa mara kwa mara kwa njia ya kujamiana au kujichua inaweza kusababishwa na vitu vingine vinayochochea afya njema, kama vile mlo kamili na uzito wa kawaida, ambao pia huweza kupunguza hatari ya saratani, alisema Dk. John Gore, mtafiti wa mfumo wa mkojo katika Chuo Kikuu cha Washington huko Seattle, ambaye pia hakuhusika na utafiti huo.
“Sidhani kama tunahitaji kuwaambia wanaume kwamba iwapo ‘hutaitumia hii, utajiju!’’ Gore alisema kwa njia ya barua pepe.
Hata hivyo, utafiti wenye matokeo kama hayo si mpya kwani mwishoni mwa miaka ya 2000 na mwanzoni mwa miaka ya 2010 zilichapishwa tafiti kama hizo nchini Marekani na Australia.
Utafiti wa kwanza ulihusisha wanaume 29,342 nchini Marekani na wa Australia ulihusisha wanaume 2,338 na kuja na hitimisho moja kuwa kukojoa mara kwa mara huzuia uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.mapenzi.ya.chumbani.kby