Unajua Kwanini Wanawake hupenda Wanaume Warefu? - Chumba Cha Mapenzi -->

Unajua Kwanini Wanawake hupenda Wanaume Warefu?

Umewahi kubaini hilo?...Kama hukubaini basi ndio ukweli wenyewe kwamba kwa asilimia kubwa wanawake huwapenda zaidi wanaume warefu.

Bila shaka umeshawahi kusikia minong’ono kuwa wanaume warefu wana mvuto mkubwa kwa wanawake tofauti na wenzao wafupi. 
Bila shaka umewahi kuisikia hii kwa baadhi ya wanaume wakikiri kuwa wanaume warefu wanakubalika kirahisi kwa wanawake.

Nimelazimika kufanya utafiti wa kisomi ili kuona kama kuna ukweli wowote au ni maneno tu ya mitaani; aidha nikajaribu upande wa pili kwa maana ya kuzungumza na wanawake ili nisikie wenyewe wanachosema, wengi wamekiri kuwa wanaume warefu wana mvuto sana.


Baadhi yao wanadiriki hata kusema kwamba huwa wanatamani kuwatongoza, shida ni mila na desturi za kwetu haziruhusu mwanamke kumtongoza mwanamume, mwingine
akaniambia kuwa wanaume warefu wengi wao wanajiamini zaidi kuliko wafupi.
   

Pia watu warefu wanajikubali sana, wapo wengi tu wanaokubali kuwa wanaume warefu
wanakuwa ni wenye mvuto...je, wewe una maoni gani?


Mtafiti mkongwe katika masuala ya mapenzi duniani, Fisher, Helen katika kitabu chake alichokipa jina la "kwa nini tunapenda", kilichochapishwa Marekani
(ISBN 0-8050-6913-5), anasema kuna ukweli juu ya jambo hili.
Anasema imani ya wanawake wengi ni kwamba wanaume warefu wana mwonekano
mzuri. Pia kina dada wanajiona wako salama zaidi wanapoongozana na mtu mrefu tofauti wakiongozana na mtu mfupi.



Ingawa wengine wanahusisha urefu wa mwanaume na urefu wa viungo...lakini kuwa na fimbo kubwa na mwingine kuwa na fimbo ndogo, haina maana kwamba mwenye fimbo
kubwa atampiga mwanafunzi akaumiza zaidi kuliko mwenye ndogo...hapa ni suala la ujuzi tu.

Kufikiri kwamba wanaume warefu ni bora kwa sababu ya urefu wao, huenda ni imani isiyo sahihi sana, ingawa kwa kiasi ina ukweli hasa katika kimo cha mtu...mara nyingi urefu wa vidole vya mwanaume vinaweza kukupa mwelekeo wa urefu wa Mashine.


Msomi Simpson, John, ed. (1989 toleo la pili), kitabu maalumu kuhusu umbo la mwanaume, kilichochapishwa na Chuo Kikuu cha Oxford University anasema kwa kiasi fulani huwezi ukawa na vidole vifupi, halafu ukatudanganya kuwa kwingine kutakuwa
kurefu, ni ngumu!


Wanawake walio wengi huvutiwa na wanaume walio warefu...achilia mbali baadhi ya
wanawake kupenda kwa sababu ya fedha, kisaikolojia wanajisikia fahari kuwa na mwanaume mrefu.
  

Sifa zingine za wanaume wafupi ambazo wanawake wengi wanasema zinawakera ni kama,

Wivu

Inasemekana wanaume wafupi wana wivu wa kupindukia na sio kama wanaume wengine warefu hawana wivu ila wivu wao unapitiliza kiasi cha kukera kwani wivu ukizidi sana ni kero katika mapenzi.

Wanaume wengi wafupi wana sifa sana, kiasi cha kukera wanajisifia sana, na wanataka sana kuonekana, kama wapo eneo Fulani wakiingia sehemu mtajua kama kuna mtu kaingia sababu ya sifa zao na maneno yao japokuwa pia wana sifa moja ya kuwa wachechi sana.

Gubu

Hapa sasa ukichanganya na wivu ni balaaa maana mwanaume mwenye gubu ni zaidi ya mwanamke muongeaji, Gubu ni ile hali ya kukosoa kila kitu,kila kitu  kibaya, yeye haridhiki na chochote na hata utaonekana huwezi chochote akiwa karibu, hilo gubu au hata kama kila kitu kipo sawa atatafuta sababu ya kuongea tu.

Wanajidai Wanajua  kila kitu. ( Much know)

Much knows, hapa bwana unakutana na mtu  kila kitu anajua yeye, ni kero sababu akiwa mbele za watu atataka kila mtu ajue anajua nini kama inaongelewa siasa, mpira au mapenzi yeye fundi wa kila kitu, kitu ambacho kiukweli kinakera sana wakati mwingine.

Muonekano/ Mvuto

Wanawake wengi wasema wanaume wafupi hawana mvuto sana, kama wanaume warefu, kwahiyo hiyo ni moja ya sababu ya wao kutotaka kutoka na wanaume wafupi, japokuwa sio wanaume wote wafupi hawana mvuto.

Japokuwa inasemekana siku hizi hakuna anae angalia urefu wako uzuri wako watu wanangalia sana mfuko wako tu, hayo ni maneno ya mitaani watu wanaongea. Ila kumbuka kama umependwa kwa Pesa hayo sio mapenzi ila ni Biashara .