Mpenzi wako amepoteza msisimko na wewe, hiki ndicho cha kufanya - Chumba Cha Mapenzi -->

Mpenzi wako amepoteza msisimko na wewe, hiki ndicho cha kufanya



WAPO baadhi ya watu waliokwenye uhusiano na wenzi ambao wamepoteza msisimko wa mapenzi. Yaani wanashindwa kuwa na uwezo wa kupenda
. Upo uwezekano kwamba, hukumwelewa vizuri mpenzi wako mwanzoni, lakini sasa unagundua kwamba amepoteza uwezo wa kupenda.
Suala la kushindwa au kupunguza msisimko wa kupenda ni ugonjwa! Lakini baadhi ya wahusika hufahamu tatizo hili na wengine hawafahamu. Wanaofahamu ni vigumu sana kueleza moja kwa moja kwamba wanakabiliwa na tatizo hili. Ni vigumu sana kugundua hili mapema, lakini ukimchunguza na kuwa mkweli kwake, ni rahisi kukueleza ukweli huu uliojificha moyoni mwake.
Pengine wakati unakutana naye, alikukatalia akisema muda wa kuwa na mpenzi bado, lakini ukaendelea kumsumbua na kukukubalia, mwisho ukagundua hafurahii uhusiano wenu.
Hili huwa tatizo kubwa sana kwa walio wengi. Wakati mwingine yawezekana ukawa unafanya bidii ya kumshawishi mpenzi mpya lakini akawa katika tatizo hili. Kila siku anakuzungusha, lakini siku moja akaamua kukueleza ukweli, kwamba anashidwa kukupenda! Huyu ni mzuri zaidi kwako, maana angalau sasa anakuwa amefahamu tatizo lake na amekupa nafasi ya kulijua, sasa wajibu wako unakuwa kumpa tiba timilifu.

Ni nini hasa?

Tatizo la kutokuwa na uwezo wa kupenda, limekuwa likiwasumbua wengi sana siku hizi (hasa wanawake). Sababu kubwa zaidi ni kuwa na uhusiano wenye historia mbaya katika kipindi kilichopita!
Mwanamke aliyeachwa na wanaume watatu kwa kipindi cha miezi miwili, hawezi kuwa na uwezo wa kupenda kwa moyo zaidi kama yule ambaye ndiyo kwanza anaanza uhusiano.
Mwanamke aliyeachwa na mwanaume wake aliyedumu naye kwa miaka minne, anaweza kuwa bora zaidi katika uhusiano mpya akitaka kuokoa maisha yake ya kimapenzi kuliko yule ambaye ametoswa mara nyingi zaidi.
Kisaikolojia, zipo sababu nyingi zinazoelezwa kwamba zinachangia sana kumfanya mtu apoteze uwezo wa kupenda. Lakini sababu kubwa zaidi zilizotajwa ni hizi hapa chini;
MOSI: Anahisi havutii sana. Mara nyingi wasichana wakiachwa, huchukulia kwamba huenda hawana mvuto sana. Kwahiyo anahisi hata kama atakupenda, akitokea mwenye mvuto zaidi yake, utamtosa kama alivyofanya aliyepita!
PILI: Huogopa ugonjwa wa moyo. Inawezekana ameshaumizwa sana huko nyuma na kila anapokuangalia anahisi kuteswa tena na hivyo anaogopa tena kupata ugonjwa wa moyo! Ana mashaka, hana amani na mapenzi tena, sababu kubwa ni historia iliyopita.
TATU: Anakuwa na mawazo kwamba, yawezekana na wewe ni sawa na mpenzi wake aliyepita. Lakini kubwa zaidi ni kwamba, mtu akiwa katika athari, akili yake yote inamwambia kwamba wote wanaweza kuwa sawa na waliopita!
…uking’atwa na nyoka, hata unyasi ukikugusa unashtuka rafiki zangu!

NAMNA YA KUMTAMBUA

Ni afadhali uwe katika hatua za kumfuatilia, kabla hujajua chochote ukagundua wazi kwamba, huyu ana tatizo la kupenda, lakini ukishaingia katika uhusiano naye, ni vigumu sana kujua, maana unaweza kuhisi anakudharau kumbe mwenzio mgonjwa!
Lakini hapa, zipo njia za kitaalamu kabisa ambazo zinaweza kukufanya ugundue mpenzi wako ana tatizo la ugonjwa wa kupenda! Hebu tuone…
Msiri sana
Sifa ya kwanza kabisa ni kwamba, hataki kukupa nafasi ya kumjua vizuri, anakuogopa, maana ukijua udhaifu wake unaweza kumtenda na kumfanya aishi mpweke kwa mara nyingine. Ni msiri sana, hataki ujue ratiba zake na mambo yake mengi anafanya kwa kushtukiza.

Simu yako haimshtui

Hayupo katika penzi la msisimko, kwahiyo hata akiona simu yako anashtuka na kuogopa kupokea haraka. Hana amani ya moyo. Hapendi kukusikia ukisema; “I love you baby!” maana anahisi kama unamuumiza tu!
Kwahiyo unaweza kumpigia simu ikaita kwa muda mrefu sana bila kupokea na hata akipokea, sauti yake huwa haina msisimko wa mahaba. Ni rahisi sana kumsikia akisema: “Nakusikiliza…ulikuwa unasemaje?”
Kauli hiyo inatosha kabisa kukuthibitishia kwamba upo na mwenzi ambaye hana msisimko kabisa na wewe.