JINSI YA KUJINASUA KWENYE MATESO YA MAPENZI
June 15, 2019
Edit
NI Jumatatu nyingine mpenzi msomaji wangu. Mungu ametujalia uzima, kama upo na tatizo lolote basi usikate tamaa Mungu atakufanyia wepesi na utarudi katika hali yako ya kawaida. Kama ilivyo ada, hapa huwa tunazungumza yahusuyo mahusiano. Tunazijadili kwa pamoja changamoto za mahusiano na kuzipatia majibu kwa pamoja. Kwenye ulimwengu huu wa sasa, matatizo kwenye masuala ya mahusiano yamekuwa mengi.
Usaliti umeshika hatamu, watu wanafanya mambo bila aibu. Uaminifu umepungua hivyo kuwafanya wenza waingie kwenye maumivu ya mapenzi. Mtu anakuwa haridhiki, anakuwa na huyu huku bado anamtamani mwingine.
MAPENZI NI STAHA
Ndugu zangu, ni lazima tujifunze kwamba mapenzi yanahitaji staha. Mapenzi yanahitaji kujitambua na mtu kuridhika. Kuamua kwamba sasa nina uhusiano fulani basi hakuna sababu ya kuwa na mtu mwingine. Kila anayeaminiwa anapaswa na yeye kutengeneza mazingira ya kuaminika.
Kutokana na watu wengi kutokuwa waaminifu au kuendekeza tamaa, tunashuhudia watu wengi wakijikuta wameingia kwenye maamuzi ambayo hawakuwahi kuyawaza. Mtu anampenda mpenzi wake lakini kutokana na vituko anavyofanyiwa, anashindwa kujizuia. Matokeo yake naye anasaliti.
TUJIFUNZE KIDOGO KWA MFANO
Rafiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mary, alinitumia ujumbe mfupi kunieleza kuwa anateseka sana kwenye uhusiano wake ambao hauna hata muda
ili kweli aweze kuwa mwenza wako wa maisha. Tumia kila mbinu kumbadilisha kama kweli unampenda, usiwe mwepesi wa kukata tamaa. Jitahidi kumtengenezea mazingira ajione kwamba anachokifanya si sahihi na pengine anajidhalilisha. Ifike mahali aone kwamba anakukosea kufanya anayoyafanya bila wewe hata kutumia nguvu.
ANGALIZO
Ukiona umefanya hivyo kwa muda mrefu na makosa yamekuwa yakijirudia, anza kumuepuka taratibu. Hii inasaidia wakati mwingine kumfanya mtu ashtuke kwamba anapoteza mtu sahihi maishani mwake, akilibaini hilo atarudi na asipofanya hivyo basi wewe endelea na maisha yako.
Usikubali kuishi na mtu ambaye ana mambo mazito ambayo hayabadiliki. Mtu ambaye ni mhuni, malaya na ambaye hataki kubadilika kitabia haifai kudumu naye muda mrefu. Kweli muweke karibu, muelekeze taratibu lakini ukiona umefanya hivyo kwa muda mrefu na haelekei basi achana naye.