KAMA UNA MOYO MWEPESI USISOME STORY HII,WENGI WAMELIA SANA !!
May 16, 2019
Edit
Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu
aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na
kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu
alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari
kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha
anaumizwa. Nilishindwa hata namna ya kuanza
kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili
ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.
Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu.
Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake
aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu swali
lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na
akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule,
hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa
kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini
kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa hakika
nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha;
alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilihamia
kwa Mary. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote
yalikuwa kwa Mary. Kwa kweli nilimdharau mke wangu!
Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa,
niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke
wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa
30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana
vipande vipande.
Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana
mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa
muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza
kurudi nyuma kwa sababu Mary aliuteka moyo wangu
kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti
mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia.
Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu.
Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa
majuma kadhaa na sasa limeendelea kuimarika na kuwa
jambo la hakika zaidi.
Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana
nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani.
Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda
moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara
moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula
raha za kufa mtu na Mary
Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado
akiandika. Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na
kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya
talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu
lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa
kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika
kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye
tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa
kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo
lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia
kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo
hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya
kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo kwangu, nilikubali
mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada,
aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate
yetu hasa siku ya harusi yetu. Akaniomba na kunisihi
kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe
nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa
kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa.
Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro
nilikubaliana na masharti yake ya ajabu.
Nilimsimulia Mary kuhusu masharti ya kuachana na
mke wangu. Mary alicheka sana, aliona ni ujinga. ‘Hata
akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’,
alisema Mary tena kwa dharau. Mimi na mke wangu
hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya
kumtaliki. Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza
sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana na kupiga
makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama
mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni
moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni,
halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi
nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema
kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu
ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia
vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba.
Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami
nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili,
zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani
pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye
blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa
makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua
hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na
nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula
urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini
namfanyia hivi.
Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu
zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na
tumeishi kwa miaka kumi sasa. Siku ya tano na ya sita
ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea
upya. Sikumwambia Mary kuhusu jambo hili. Kadiri
mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke
wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya
kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi.
Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua
mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna,
‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua
kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo
maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo
likanichoma... mke wangu ana uchungu na maumivu
makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa
kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema
‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’.
Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo
la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara
mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo
mkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo
katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi
mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka
mlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka
shingo yangu kwa upendo. Nilimkumbatia mwili wake;
ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi
wake ulinitia mashaka.
Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga
hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni.
Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba
maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini….
Nikashuka garini hata bila kufunga mlango. Maana
nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua....
nikapand ngazi. Mary alifungua mlango nikamwambia,
‘Samahani, Mary, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’.
Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa
changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?’ Nikaondoa mkono wake
kichwani kwangu. ‘Samahani, Mary, nimesema sitaki
kumtaliki mke wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na
furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu,
mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani.
Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu
nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu,
nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo
kitakapotutenganisha.’
Ikawa kama Mary alizinduka usingizini. Akanizaba kibao
cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia.
Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye
duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili
ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye
kadi. Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila
asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenganisha”.
Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu,
tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani,
nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani.
Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani
kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu
nilihamishia akili yangu kwa Mary. Alijua kwamba
angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na
mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema.
Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume
mwema.
Mungu nisaidie Nisifike huku mimi.
Kama Stori Hii Imekugusa Na Ungependa Marafiki Nao
Waisome Basi Unaweza kusambaza (share na wenzako)